Zambia yafunga mipaka na Tanzania leo


0

Zambia imechukua hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona kwa kufunga mpaka wake na nchi ya Tanzania kuanzia leo Jumatatu. 

Hii inakuja baada ya kuwa na maambukizi mengi kwa baadhi ya wafanyabiashara wa ngono na madereva wa Malori kwenye miji ya mipaka nchini humo.

Waziri wa afya nchini humo Chitalu Chilufya anasema wafanyabiashara wa ngono wamekuwa wakitoa ushirikiano katika kutoa taarifa zinazohusiana na wagonjwa wapya wa virusi vya corona kwenye mpaka wa Nakonde.

Amesema watu 76 kati ya 85 walioripoti visa vipya katika eneo hilo  walikua ni wafanyabiashara wa ngono au madereva wa malori.

Zambia imethibitisha visa 267 vya maambukizi ya Covid-19 na vifo saba.

Wiki iliyopita Rais Edgar Lungu alitangaza kufunguliwa tena kwa migahawa ya chakula, kumbi za kamari na za mazoezi ya mwili-(gym) baada ya nchi hiyo kuwa chini ya amri ya kutotoka nje kwa mwezi mmoja.


Like it? Share with your friends!

0