WHO yaonya Waafrika 190,000 kufariki kwa COVID -19


0

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema mlipuko wa virusi vya corona unaweza kusababisha vifo kwa Waafrika takribani 190,000 ndani ya mwaka mmoja tangu ugonjwa huu uanze kama utashindwa kudhibitiwa

Mkurugenzi wa WHO Afrika, Dkt. Matshidiso Moeti amesema kuna uwezekano ugonjwa wa corona hautosambaa kwa kasi barani humo kama ilivyokuwa kwa mataifa mengine duniani

Ameongeza kuwa maambukizi yataenea zaidi katika maeneo yenye joto

Mkurugenzi huyo amezitaka Serikali kuweka mikakati ya kupima virusi vya corona, kutafuta waliokuwa karibu na wagonjwa, kuwekwa karantini walio na maambukizi na vilevile kuwatibia.

Taarifa hii inakuja ikiwa baadhi ya nchi za Afrika zenye watu wengi kama Afrika kusini, Naijeria na Ivory Coast wakilegeza sheria ya kuzuia watu kutoka nje 

Awali WHO ilitabiri Waaafrika Milioni 29 hadi 44 wanaweza kupata maambukizi ya corona kwa mwaka mmoja na watu Milioni 5.5 wanaweza kuhitaji tiba Hospitali, idadi ambayo ni kubwa kuliko uwezo wa sekta za afya katika nchi nyingi.


Like it? Share with your friends!

0