Wazungu washtakiwa kwa kumuua Mmarekani mweusi


0

Baba na mtoto wake wa kiume wamekamatwa na kushtakiwa katika jimbo la Georgia nchini Marekani, kwa kosa la kumuua kwa kumpiga risasi kijana Ahmaud Arbery, Mmarekani mweusi aliyekuwa akifanya mazoezi ya kukimbia barabarani.

 Gregory McMichael (64) na mwanaye Travis McMichael (34) anayedaiwa kufyatua risasi iliyomuua Arbery, walikamtwa jana usiku na wapo chini ya ofisi ya uchunguzi nchini humo na mmoja wa wapelelezi anasema, wawili hao wanashtakiwa kwa kosa la mauaji na kufanya shambulio.

Februari mwaka huu, Arbery alikuwa akifanya mazoezi ya kukimbia barabrani, ndipo watuhumiwa hao ambao ni wazungu walimvamia na kumshambulia kwa risasi.

Kitendo cha kucheleweshwa kushtakiwa kwa watuhumiwa hao baada ya kutekeleza tukio hilo, kulizua mijadala na hasira nchini humo na katika mitandao ya kijamii.

Mtuhumiwa Gregory akitoa maelezo polisi alidai kuwa walimuona Arbery akikimbia na kumfananisha na mtuhumiwa wa uvunjaji wa nyumba, hivyo yeye na mwanae wakiwa kwenye gari walimtaka asimame ili waongee naye lakini alianza kumshambulia mwanaye (Travis), kitendo kilichowafanya wampige kwa risasi

Mama wa Arbery anasema haamini kama kweli mwanaye alifanya uhalifu hadi kufikia kuuawa na hakuwa na silaha yoyote.

 


Like it? Share with your friends!

0