Waziri akutwa na COVID 19.


0

 

LIBERIA

Waziri wa elimu nchini Liberia Ansu Sonii na naibu wake Latim Da-thong wamekutwa na maambukizi ya virusi vya corona na wanaendelea na matibabu wakati huu ambao wizara inajiandaa kufungua shule baada ya kufungwa kufuatia janga la virusi hivyo.


Kwa mujibu wa gazeti la Front Page Africa la nchini humo, waziri Ansu Sonii anatibiwa katika hospitali ya jeshi wakati naibu wake Latim Da-thong yeye alisafirishwa hadi nchini Ghana baada ya hali yake kuwa mbaya

Waziri wa habari Lenn Eugene Nagbe amenukuliwa na gazeti hilo akisema kuwa kwa sasa hali ya naibu huyo inaendelea vizuri lakini alikanusha taarifa za kuwa Waziri wa elimu pia amepelekwa nchini Ghana kwa matibabu.

Liberia inajumla ya visa 652 vya maambukizi ya virusi vya corona na vifo 34

Siku ya jumatatu nchi hiyo ilitangaza kufungua shule kwa wanafunzi wa daraja la 12 ambao wanajiandaa na mitihani kuanzia jumatatu ya June 29, 2020.


Like it? Share with your friends!

0