Watu 65 wauawa Nigeria


0

Takribani watu 65 wameuawa baada ya watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Boko Haram kuwashambulia katika hafla ya mazishi kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Afisa wa Serikali wa eneo hilo Mohammed Bulama ameiambia Televisheni ya taifa ya nchi hiyo kuwa , watu 21 waliuawa wakati wa mazishi hayo yakiendelea katika kijiji cha Badu, katikati mwa jimbo la Borno siku ya Jumamosi.

Ameongeza kuwa Wakati wengine wakiwa wanakimbilia katika eneo hilo katika juhudi za kuwaokoa walioshambuliwa, watu 44 zaidi wakauwa na kufanya idadi ya waliopoteza Maisha kufikia 65.

Wanamgambo kumi waliuawa katika mapigano hayo ambayo yametajwa kuwa yalikuwa ya kulipiza kisasi, baada ya wanakijiji na makundi ya ulinzi wa raia kupambamana dhidi shambulizi la Boko Haram, katika eneo hilo wiki mbili zilizopita na kuwauwa wapiganaji 11.

Jeshi la Nigeria halijatoa taarifa yoyote ya haraka kuhusu shambulizi hilo.


Like it? Share with your friends!

0