Watoto milioni 258 wakosa shule


0

UNESCO

Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekadiria kuwa takribani watoto milioni 258 hawakwenda shule mwaka 2018, ikiwa ni sawa na asilimia 17 ya watoto wote duniani.

Ripoti mpya ya hali ya elimu duniani ya UNESCO imeonesha kuwa takriban asilimia 90 ya walioathiriwa na hali hiyo ni kutoka katika nchi za Afrika zilizoko Kusini mwa Jangwa la Sahara na Asia huku umasikini ukitajwa kuwa sababu kubwa inayoathiri fursa za elimu katika maeneo hayo.

Pia, ripoti hiyo imeeleza kwamba mamilioni ya wavulana na wasichana wamekuwa wakibaguliwa katika mifumo ya elimu kwa sababu ya asili zao, mila, desturi na ulemavu kwa baadhi yao.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Audrey Azoulay amesema janga la corona limeathiri zaidi shughuli za elimu, na kwamba tatizo hilo la kiafya linaweza kuwa chanzo cha kuwafanya watoto wengi wasirudi shuleni hasa wasichana kutoka familia masikini.

Chanzo DW.

 

 


Like it? Share with your friends!

0