Wanafunzi Hong Kong waandamana wakiwa wameficha sura


0

Mamia ya wanafunzi waliovaa sare za shule na kujifunika nyuso mjini Hong Kong, China, wameandamana leo wakiwa wameshikana mikono wakiunga mkono maandamano ya kuipinga serikali.

Naye mwanaharakati wa Hong Kong anayepigania demokrasia, Joshua Wong, 

ameachiliwa huru kwa dhamana leo ikiwa ni saa 24 baada ya kukamatwa akiwa uwanja wa ndege mjini Hong Kong, 

akielekea Ujerumani kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana.

Kwa sasa Wong yuko njiani kwenda Ujerumani. Maandamano ya miezi mitatu kuhusu muswada ambao sasa umefutwa, yamepanuka na kinachotolewa wito sasa ni mabadiliko ya demokrasia mjini humo.


Like it? Share with your friends!

0