Waitara awaonya walimu kudai nyongeza ya mishahara


0

BUNGENI:Serikali imesema walimu hawapaswi kudai nyongeza ya mwaka ya mshahara kwa miaka ambayo nyongeza hiyo haikutolewa.

Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mwita Waitara, ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma,  wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Zainab Mussa Bakar (Chadema), ambaye katika swali lake alitaka kujua

“Walimu nchini wameingia mkataba na mwajiri wao ambao pamoja na mambo mengine unaonyesha uwepo wa nyongeza wa mshahara kila ifikapo Julai, lakini tangu Serikali ya awamu ya tano iingie madarakani, hawajapewa stahiki hizo, je ni lini walimu watalipwa malimbikizo hayo?”

Akitoa majibu ya swali hilo Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara alisema Serikali imekuwa ikitekeleza miongozo mbalimbali, kuhusu maslahi ya walimu zikiwamo nyongeza za mwaka za mishahara kulingana na utendaji wa mhusika na tathmini ya kila mwaka.

“Kwa mujibu wa kanuni E.9 (1) ya kanuni ya kudumu katika utumishi wa umma za mwaka 2009 toleo la tatu, nyongeza ya mwaka ya mshahara haipaswi kuombwa au kudaiwa na walimu, bali serikali ndiyo yenye uamuzi wa kutoa au kutotoa nyongeza hiyo kutokana na sera za kibajeti kwa mwaka husika.


Like it? Share with your friends!

0