Uncategorized

Virusi ‘dizaini’ ya corona vyagundulika China


0

CHINA

Wanasayansi wamebaini uwepo wa aina mpya ya virusi vinavyosababisha mafua nchini China, ambavyo vinahofiwa kuwa huenda vikasababisha janga kwa dunia.

Virusi hivyo vinatajwa wakati dunia inapambana na virusi vya corona vinavyoaminika kuanzia nchini humo na kuenea kwingineko duniani.

Wataalamu hao wamesema virusi hivyo vilivyobainika hivi karibuni, vinapatikana kwa nguruwe ingawa kuna uwezekano wa kuongezeka kwa haraka na kuhamia kwa binadamu.
Licha ya kuwa hadi sasa havijawa tishio, lakini imeelezwa kuwa kuna dalili kuwa vinaweza kuwaathiri binadamu, hivyo kuhitaji ufuatiliaji wa karibu.

Kutokana na upya wake, virusi hivyo vitakuwa changamoto kwa sababu miili ya watu itakuwa na uwezo mdogo au kutokuwa na uwezo kabisa wa kukabiliana navyo.

Mara ya mwisho dunia kukumbwa na janga la mafua ilikuwa ni 2009 ambapo mafua ya nguruwe yalianzia nchini Mexico.

Aina mpya ya mafua iliyobainika nchini China ina ufanano kiasi na mafua ya nguruwe ya mwaka 2009, lakini watafiti wanasema kwa kiasi fulani yanatofautiana.

 


Like it? Share with your friends!

0