Viongozi wajitokeza kuaga miili ya wafanyakazi wa Azam Media


0

Viongozi na wanasiasa nchini Tanzania wamejitokea leo asubuhi Jumanne Julai 9, 2019 kuaga miili ya wafanyakazi watano wa Azam Media waliofariki dunia jana katika ajali ya gari aina ya Toyota Coaster iliyogongana na lori uso kwa uso.

Ibada ya mazishi ya wafanyakazi hao inafanyika katika viwanja vya kampuni hiyo iliyopo Tabata TIOT barabara ya Mandela, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya viongozi na wanasiasa hao ni kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe; mbunge wa Ilala (CCM), Mussa Azzan Zungu; mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na naibu katibu mkuu wa chama hicho, Magdalena Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua.

Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba; mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda; naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni; Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe.

Mbunge wa Segerea (CCM), Bona Kimoli; waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii, Khamisi Kagasheki, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Crescetius Magori.

Waliofariki dunia katika ajali hiyo ni Salim Mhando, Florence Ndibalema, Said Haji, Sylvanus Kasongo na Charles Wandwi.

Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ambao pia ni wafanyakazi wa kampuni hiyo ni Mohamed Mwinshehe, Mohamed Mainde na Masawe.


Like it? Share with your friends!

0