Vifo vya Saratani vyatajwa kuongezeka ifikapo 2030.


0

Vifo vitokanavyo na ugonjwa wa saratani ya matiti vinatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 80 ifikapo mwaka 2030.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Daisy Majamba, alisema ugonjwa huo bado ni tishio kwa wanawake na inakadiriwa ifikapo 2030, idadi ya wagonjwa wapya itaongezeka kwa asilimia 82 jambo ambalo linahatarisha ustawi wa afya nchini.

“Tusipochukua hatua mapema za tahadhari, hali ya saratani ya matiti inaweza kuwa mbaya zaidi, ndiyo maana Serikali inashirikiana na sekta binafsi kulitatua,” alisema Daisy.

Alisema saratani ya matiti kwa sasa inashika nafasi ya pili kati ya saratani zinazosababisha vifo zaidi ukiacha ile ya mlango wa kizazi.

“Tunahitaji kuwajengea uwezo Watanzania, hasa kwa kutoa elimu ya ufahamu wa ugonjwa huo kwa wanafunzi mashuleni ili kuwe na uelewa wa kutosha katika jamii,” alisema Daisy.


Like it? Share with your friends!

0