Utata juu ya madai ya kubaka ya D’banj


0

Mawakili wa mwanamke anayemtuhumu mwanamuziki wa Naijeria Dapo Oyebanjo maarufu kama D’banj kwa ubakaji, wamelalamikia mamlaka za nchini humo kwa kumkamata mteja wao Seyitan Babatayo na kudai kuwa kitendo hicho ni kinyume cha sheria.

Mapema mwezi huu mwanamke huyo Babatayo alidai mwaka 2018 alibakwa na nyota huyo wa wimbo wa Falling in Love anayefahamika zaidi kwa jina la D’banj.

Wakili wa mwanamuziki huyo anasema mteja wake amekataa shutuma hizo na alimuandikia barua mwanamke huyo kumtaarifu kuwa watachukua hatua za kisheria dhidi yake kama hatofuta mashtaka hayo.

Mapema juma hili mwanamke huyo Seyitan Babatayo ambaye ni mwanamitindo alidai kukamatwa na polisi na kuachiwa kwa dhamana ingawa wakili wake anasema hajui sababu ya mteja wake kukamatwa na wameandika malalamiko yao.

Babatayo alitoa madai ya kubakwa na mwanamuziki huyo June 8, 2020 na kusema tukio hilo lilitokea katika moja ya hoteli iliyopo mjini Lagos mwaka 2018.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na maandamano nchini Nigeria baada ya madai kadhaa ya ubakaji kuripotiwa.

Magavana wa majimbo takriban 36 nchini humo waliungana pamoja juma lililopita na kutangaza hali ya tahadhari dhidi ya ukatili wa kijinsia


Like it? Share with your friends!

0