Utajiri wa Kabuga ulivyotumika kwa mauaji Rwanda


1
1 point

 

Mahakama nchini Ufaransa imekataa ombi la mtuhumiwa wa mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda, Felicien Kabuga, aachiwe kwa dhamana wakati akisubiri uamuzi kuhusu mahali kesi yake itakaposikilizwa.

Felicien Kabuga alizaliwa mwaka 1935, kata ya Byumba, wilaya ya Gicumbi, nchini Rwanda. Kabuga aliyezaliwa katika familia maskini alianza kujenga utajiri wake alipoingia katika biashara ya mitumba na sigara. Hatimaye Kabuga akiingia kwenye biashara ya zao la chai na kuhamia Kigali ambapo aliendelea na biashara ya mazao na inasemekana biashara zake zilifika katika nchi jirani. Binti zake wawili Kabuga waliolewa na watoto wa  Rais wa wakati huo wa Rwanda Habyarimana na hivi kumweka karibu zaidi na kikundi kidogo cha utawala. Inasemekana Kabuga pia alikuwa sehemu ya kikundi cha Interhamwe na inasemekana kuwa alitumia fedha zake kuendesha redio na televisheni Libre des Milles Collines na gazeti la Kangura lililotumika kuchochea chuki dhidi ya raia wa Tutsi.

Kabuga anatuhumiwa na mahakama kufadhili mipango ya kufanya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, yaliyoangamiza maisha ya watu zaidi ya 800,000, wengi wao wakiwa kutoka jamii ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa kadri katika muda wa siku 100.

Alifika mahakamani akisukumwa kwa kiti cha magurudumu, na kuiomba mahakama imwachiwe kwa mdai kuwa ana afya mbovu na uzee wa miaka 87, lakini rekodi zinaonesha kuwa na miaka 85.

Mwendesha Mashtaka wa chombo cha kimataifa kinachofuatilia kesi za uhalifu, Serge Brammertz, amesema ikiwa atahamishwa  nchini Ufaransa, Kabuga atafikishwa katika mahakama ya chombo hicho iliyopo mjini Arusha, nchini Tanzania.


Like it? Share with your friends!

1
1 point