UNICEF yaomba dola bilioni 1.6 kunusuru watoto


0

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), limeomba mchango wa dola bilioni 1.6 ambazo ni zaidi ya mara mbili ya kiasi cha fedha ilichoomba miezi miwili iliyopita, ili kuwasaidia watoto wanaokumbwa na mizozo ya kibinadamu na ambao kwa sasa wanapambana na virusi vya corona.

UNICEF imesema kuanzia Machi mwaka huu imepokea dola milioni 215 na kwamba utafiti wake umeonyesha kuwa watoto bilioni 1.8 wanaishi katika mojawapo ya nchi 132 ambazo zina baadhi ya vikwazo vilivyowekwa na serikali kwa ajili ya kupambana na virusi vya corona.

Shirika hilo linafanya kazi katika nchi ambazo zinakabiliwa na mizozo ya kibinadamu kwa kuzuia kuenea kwa virusi vya corona, na kupunguza athari ya virusi hivyo kwa uwezo wa raia kupata matibabu, chakula, maji, elimu na ulinzi.


Like it? Share with your friends!

0