Unataka kupunguza uzito? Fuata ushauri huu!


-1
-1 points

Utafiti huo uliofanywa na wasomi katika Chuo cha Wanawake cha Doshisha (Doshisha Women’s College of Liberal) huko Kyoto nchini Japan, ambapo wamechunguza jinsi matumizi ya mchele yanavyoweza kupunguza ongezeko la uzito kupita kiasi katika nchi 136, na idadi ya watu zaidi ya milioni moja kuhusishwa.

Watafiti walichambua kila aina ya bidhaa za mchele, ikiwa ni pamoja na mchele mweupe, mchele wa kahawia, na unga wa mchele, kwa kutumia takwimu kutoka Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa.

Timu hiyo pia ilitazama mitindo ya maisha na sababu za kiuchumi katika nchi ilikopita, ikiwa ni pamoja na elimu, matumizi ya nishati ya jumla, bidhaa za ndani kwa kila mtu, kiwango cha sigara, na matumizi ya afya.

Waligundua kuwa kiwango cha ongezeko la uzito kupita kiasi kilikuwa cha chini katika nchi zilizo na matumizi makubwa ya bidhaa za mchele, hata baada ya kuzingatia mambo mengine ya hatari.

Mashirika yaliyotajwa yanaonyesha kwamba kiwango cha uzito kupindukia ni cha chini katika nchi ambazo hula mchele kama chakula kikuu. Kwa hivyo, chakula cha Kijapani au mlo wa chakula cha asili cha ki ASIA unaweza kusaidia kuzuia ongezeko la uzito wa kupindukia, “amesema Profesa Tomoko Imai mmoja ya watafiti.

Sambamba na hilo, utafiti unaonyesha kwamba hata ongezeko la wastani katika matumizi ya mchele kunaweza kusaidia kupunguza ongezeko la uzito. Kwa mfano, kama kila mtu atakula robo ya ziada ya kikombe, au gramu 50, za mchele kwa siku, ni dhahiri ongezeko la watu wenye uzito kupindukia litapungua kwa asilimia moja.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, kuna wastani wa watu wenye umri wa miaka 18 na kuendelea ambao wanajulikana ama kutambulika kua na uzito kupitiliza.

Hata hivyo nchi tano zinazoongoza kwa matumizi ya bidhaa za mchele ni Bangladesh iliyofuatiwa na Lao, Cambodia, Vietnam na Indonesia. Canada ilikuwa nafasi ya 77 kwenye orodha ya matumizi ya bidhaa hizo.

Utafiti huo umeonya kuwa kula wali ama kiwango cha kupitiliza cha bidhaa za mchele huenda kikasababisha  kisukari, ugonjwa wa moyo na kiharusi.

 


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points