Ukileta fujo unabanwa mbavu – Dk. Hamis Kigwangalla


0

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania, Dk Hamis Kigwangalla amesema wanaharakati wanaopinga mradi wa kufua umeme wa Stigler’s Gorge watafanyiwa fujo zisizoumiza kabla hawajafika kwa Rais wa Tanzania, John Magufuli lakini ikibidi watabanwa mbavu.

Dk Kigwangalla ametoa kauli hiyo leo Jumanne Julai 9, 2019 wakati wa uzinduzi wa Hifadhi Taifa ya Burigi- Chato mkoani Geita ambayo imetokana na kuunganishwa kwa mapori ya akiba ya Kimisi, Burigi na Biharamulo.

Amesema Rais Magufuli ndiye mhifadhi namba moja anayetekeleza kwa vitendo na hahitaji mtu yeyote kutoka ndani na nje ya nchi kuja kutufundisha namna ya uhifadhi.

“Ulipotia nia ya kuwekeza katika mradi wa kufua umeme katika mbuga ya Selous kuna wanaharakati walianza kupiga kelele wa ndani na wa nje kana kwamba hifadhi ni ya kwao au wanajua kuhifadhi kuliko wewe,” amesema

Amesema mradi ule ni wa siku nyingi hata wakati mbuga hiyo inaomba kuidhinishwa kuwa miongoni mwa urithi wa dunia UNESCO walielezwa kuna mpango wa mradi huo na waliridhia hivyo hata baada ya mradi hadhi itaendelea kuwa ile ile.

“Wanaharakati ambao wanapenda kujionyesha…wakiendelea kuleta chokochoko kupitia mawakala wao mbalimbali wa kisiasa na harakati tutaanza nao sisi kabla ya kukufika kwako, tutawafanyia fujo zisizoumiza ikibidi kuwabana mbavu tutafanya hivyo,” Dk Kigwangalla


Like it? Share with your friends!

0