Uchovu wa shahidi waahirisha kesi ya akina Mbowe


0

Kesi namba 112/2018, inayowakabili viongozi wakuu wa kuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na baadhi ya wabunge, imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi kesho, baada ya  shahidi wa nane, Benard Nyambalia kuomba udhuru kwa uchovu.

Awali upande wa mashtaka uliomba kesi iahirishwe kwa muda, kwa kuWa kuna jambo la kujadili kati ya Hakimu na Mawakili wa upande wa utetezi.

Awali, kuliibuka mzozo baada ya washtakiwa, Freeman Mbowe, Mchungaji Peter Msigwa na John Heche kusimama wakitaka mwongozo wa Hakimu, mara baada ya mawakili wa serikali kutowaleta mashahidi wengine huku aliyeletwa akisema kwamba ana uchovu, hivyo anaomba udhuru.

Kwa upande wake, Msigwa alidai kuwa hata wao wameacha mambo ya msingi vikiwemo vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma, huku Heche akihoji endapo mahakama hiyo inawafunga kabla ya hukumu, kwa kuwa wamekuwa wakipoteza muda na gharama nyingi.  

Katika kutoa msimamo wake, Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba, amewataka mawakili wa serikali kuwaleta mashahidi hapo kesho, kwa kuwa shauri hilo limechukua muda mrefu. 

Shauri hilo lilipangwa kusikilizwa kwa siku tatu mfululizo kuanzia leo.


Like it? Share with your friends!

0