Ubaguzi wa rangi ulivyowagawa Wajapani


0

Ubaguzi wa rangi ni janga la dunia nzima, utofauti uliopo kwenye ngozi ya mwanadamu hufanya mwingine kujiona bora zaidi ya mwenzie.

Tangu karne na karne dunia imekuwa ikipambana na masuala ya ubaguzi hasa wa rangi, kwa kiasi inaonekana kupungua, japo kwa baadhi ya maeneo au nchi bado hali ni tete.

Inaelezwa kuwa nchini Japan miaka  ya nyuma kulikithiri ubaguzi wa rangi, na utaifa kwa kiasi ambacho hata kuchangamana na walio wajapani asilia ilikuwa ni ngumu.

Waliwapa jina la HAFU watu wote waliochanganya damu kutoka mataifa mengine, waliwachukia kwa maana wengi wa HAFU walikuwa ni wenye mionekano mizuri. Upekee waliokuwa nao ndio ulipelekea kulikamata soko la mitindo nchini humo, na wana mitindo wengi hadi sasa nchini humo ni HAFU.

Haikuwa rahisi kwa machotara hao kuweza kukabiliana na hali hiyo, mmoja kati ya wanamitindo wakubwa nchini humo aitwae Rina Fukushi, alisikika akisema kuwa kipindi yupo shule alikuwa akizomewa na kufuatwa nyuma nyuma yote ni kwa sababu alikuwa ni HAFU,” hali hii ingeweza kunirudisha nyuma nisifikie malengo yangu”  alisema  Fukushi.

wahamiaji na machotara waliishi kama wakimbizi, hawakuwa na nafasi sawa kama wengine, walionekana kama wasio  na haki mbele yao, mwaka 2011 ilifanyika Makala iliyopewa jina la  “HAFU: THE MIXED RACE EXPERIENCE IN JAPAN”  Makala hii inatajwa kuleta mwangaza mpya  kwao, na baadhi yao wanakiri kuona mabadiliko katika sehemu mbalimbali ambazo wanajihusisha nazo.


Like it? Share with your friends!

0