Twitter wazuia chapisho la Rais Trump


0

MAREKANI

Mtandao wa kijamii wa Twitter umeficha chapisho la Rais wa Marekani Donald Trump linalowataka polisi wa mji wa Minneapolis kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji wanaopinga kifo cha mtu mweusi George Floyd kwa madai ya kuwa unakikuka sheria za mtandao huo na kuhamasisha vurugu.

Hatua hii inakuja ikiwa maandamano hayo yanaingia siku ya tatu mfululizo huku kukiwa na vurugu pamoja na uharibifu wa mali ikiwemo kuchomwa moto kwa kituo cha polisi cha Minneapolis.

Rais Trump alichapisha ujumbe juu ya kutuma kikosi cha ulinzi cha taifa na kufuatia na ujumbe unaosema kuwa waandamanaji hao wanavunja heshima ya kumbukumbu ya George Floyd na hatoruhusu hili litokee, ameongea na gavana Tim Walz na kumwambia kikosi cha ulinzi kinaenda

Trump alimalizia kwa kuandika kuwa serikali kuu itadhibiti iwapo “uporaji utakapoanza na risasi zitaanza Asante!”

Mtandao wa Twitter unazuia chapisho hilo la Trump ikiwa ni saa chache zimepita tangu Rais Trump kutia saini agizo linalolenga kuondoa baadhi ya marufuku ya kisheria ambayo mitandao ya kijamii inazo.

Saini hiyo inampa mamlaka ya kuweka hatua za kisheria dhidi ya makampuni ya mitandao ya kijamii kama Facebook na Twitter katika sheria walizoweka katika maudhui wanayochapisha kwenye mitandao yao.


Amri hiyo inatarajiwa kukumbana na changamoto za kisheria kwani bunge la Marekani au mfumo wa mahakama lazima viusike ili kubadili sheria iliyopo sasa.

Siku ya Jumatano Trump aliishutumu Twitter kwa kuingilia uchaguzi baada ya kuongeza maelezo ya tweet mbili kama uthibitisho.

 

 


Like it? Share with your friends!

0