Tshisekedi ashtukia mageuzi Mahakamani


0

DRC CONGO

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Felix Tshisekedi, amekataa mageuzi kwenye mahakama, akisema yatadhoofisha uhuru wake na kuathiri msingi wa kanuni zinazosimamia haki.
Kumekuwepo na hali ya kutoelewana katika muungano wa utawala juu ya mapendekezo yaliyotolewa ili kufanya mabadiliko, hususan kuipatia nguvu zaidi wizara ya sheria katika kushughulikia mashitaka ya uhalifu
Tofauti hizo zilisababisha wiki iliyopita kukamatwa kwa waziri wa sheria na kusababisha waziri mkuu kutishia kujiuzulu.
Katika hotuba yake kwa taifa ya kuadhimisha miaka 60 ya uhuru wa taifa hilo kutoka mikononi mwa Ubelgiji, Rais Tshisekedi amegusia mgogoro huo, akisema hakubaliani na mageuzi yoyote kwenye mahakama.
Rais huyo aliingia madarakani Januari mwaka jana na kuunda ushirika na mtangulizi wake, Joseph Kabila ambaye bado ana nguvu kupitia wingi wa viti bungeni, baraza la mawaziri na ofisi ya waziri mkuu.

 


Like it? Share with your friends!

0