Trump kusitisha uhusiano na China


0

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kuvunja uhusiano kati ya taifa lake na nchi ya China kutokana na kushindwa kudhibiti janga la Corona.

Katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha Fox nchini Marekani, Rais Trump amesema hana hata nia ya kuzungumza Rais Xi Jinping wa China kwa hivi sasa.

Ameenda mbali zaidi na kusema anafikiria kusitisha uhusiano na taifa hilo la pili kwa nguvu za uchumi duniani kwani amesikitishwa  na kitendo cha China kushindwa kulidhibiti janga la corona. 

Amenukuliwa akisema China haikutakiwa kuruhusu janga hili litokee na janga hilo limeharibu mpango wake wa biashara na Beijing ambapo hapo mwanzo ulionesha mafanikio.

Naye waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika kuwa ‘China, nchi ambayo virus hivi vimetokea na kuruhusu ugonjwa huu kusambaa wamekataa kuonesha ushirikiano kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa wa corona.

Takwimu zinaonesha Marekani imeathiriwa vibaya zaidi maambukizi ya virusi vya corona ambapo mpaka sasa inajumla ya vifo zaidi ya 80,600.


Like it? Share with your friends!

0