TASAC yapiga marufuku tozo za ushuru wa forodha


-1
-1 points

Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (Tasac) limepiga marufuku na limeondoa tozo za ushuru wa forodha kwa mamlaka za usafirishaji wa majini zilizokuwa kero kwa huduma hiyo.

Utekelezaji huo unafanyika chini ya kifungu Na 4 cha Sheria ya Wakala wa Meli Tanzania ya mwaka 2017,  Ibara ya 14 kutokana na agizo kutoka kifungu 12(1)(d) cha ibara ya sheria ya viwango na tozo katika sekta ya usafiri wa majini nchini.

Kwa mujibu wa tangazo lilitolewa kwenye vyombo vya habari, tozo hizo nane ni kati ya dola za Kimarekani 15 na 150.

Kufutwa kwa tozo hizo kumetokana na kugundua kuwapo kwa tabia ya baadhi ya watoa huduma za usafiri wa majini kutoza tozo kwa kiwango kikubwa, na kujipangia viwango vya kutoza wanapotoa huduma bila uthibitisho kutoka kwa mamlaka na bila mahitaji ya sheria husika.

Kwa mujibu wa tangazo hilo, kuna malalamiko mengi kutoka kwa watoa huduma, kutoa majina yasiyo sahihi ya tozo za ushuru wa forodha ulioidhinishwa kwa kiwango ambacho kinasababisha kuwachanganya wateja.

Aidha, mamlaka hiyo imesema watoa huduma wote wa usafirishaji majini wanatakiwa kukataa kutoa tozo za ushuru wa forodha ambazo hazijaidhinishwa na mamlaka hiyo.

Pia Tasac imesisitiza kuwa endapo kutakuwa na ukiukwaji wa agizo hilo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa ikiwamo kusimamishwa kutoa huduma au kunyang’anjwa leseni.

Aidha, tangazo hilo limebainisha kuwa watoa huduma wanatakiwa kuripoti kwa Tasac kama itatokea wanatakiwa kulipa ushuru wa forodha usioidhinishwa.


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points