Tanzania yapokea shehena ya dawa ya Madagascar


0

 

Tanzania imethibitisha kupokea shehena ya dawa ya mitishamba kutoka Madagascar inayodaiwa kutibu corona .

Msemaji mkuu wa serikali amethibisha hilo kupitia mtandao wake wa Twitter baada ya kutuma picha ya waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi akipokea dawa hizo na kuandika  ‘Tanzania leo imepokea msaada wa dawa zinazofubaza Virusi vya Corona kutoka Serikali ya Madagascar’.

Dawa hizo zimewasili Tanzania wakati ambapo nchini Madagascar kwenyewe idadi ya wagonjwa wa corona inaripotiwa kuongezeka na kufikia watu 195 baada ya maambukizi mapya 35 kutangazwa licha ya kuwa na dawa hiyo ya mitishamba imeanza kutumika

 Mei 3 mwaka huu Rais Magufuli alisema kuwa atatuma ndege Madagascar kwenda kufuata dawa ya hiyo mitishamba na kuongeza kuwa tayari amewasiliana na Madagascar baada ya kupokea barua rasmi kutoka nchi hiyo iliyoeleza kuwa wamegundua dawa ya corona.

 


Like it? Share with your friends!

0