TANAPA yahimiza ushirikiano kukabiliana na Corona


0

Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Dk Allan Kijazi, amesema ushirikiano miongoni mwa Watanzania utachangia kwa kiasi kikubwa kuliokoa taifa na watu wake, dhidi ya athari zinazotokana na maambukizi ya virusi vya corona.

TANAPA ni miongoni mwa taasisi zilizopo kwenye sekta ya maliasili na utalii ambayo Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangalla, aliliambia Bunge mjini Dodoma jana Mei 7, mwaka huu kuwa ni miongoni mwa sekta zilizoathirika kutokana na janga la corona.

 Kwa mujibu wa Kigwangalla aliyekuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020, pamoja na kujadili na kupitisha makadirio na mapato na matumizi kwa mwaka 2020/2021, Tanapa katika kipindi cha2020/2021 ilitarajia kukusanya Shilingi Bilioni 363.9, lakini kutokana na hali inavyoendelea sasa, makisio hayo yanatarajiwa kuwa Shilingi Bilioni 64 au chini yapo.

Lakini kwenye ujumbe wake kupitia video uliosambazwa na Meneja Uhusiano wa TANAPA, Paschal Shelutete, Dk Kijazi anasema

“Homa hii imesababisha athari kubwa za kijamii, kiuchumi na katika ngazi ya familia, na hivyo kuathiri mipango mingi ambayo imekuwa ikifanyika katika ngazi mbalimbali.” Alisema Dk Kijazi 

Hata hivyo, Dk Kijazi anaamini kwamba janga la corona litadhibitiwa hapa nchini na kwingineko duniani, kisha watu kurejea kwenye mfumo wa maisha kama ilivyokuwa awali.

“Naamini kwamba tukishirikiana katika ngazi za familia, jamii na Watanzania wote, tuna uwezo wa kulitokomeza janga hili na kuyarudia maisha yetu ya awali ambayo tulikuwa tumeyaozoea, kabla ya janga hili kuingia katika nchi yetu.”Alisema Dk Kijazi 


Like it? Share with your friends!

0