Sudan yaondolewa uanachama AU


0

Umoja wa Afrika AU umesema unasitisha uanachama wa Sudan, katika Umoja huo hadi pale madaraka ya nchi hiyo yatakapohamishwa kwa mamlaka itakayoongozwa na raia.

Umoja huo hapo kabla ulihimiza utaratibu mzuri wa kukabidhi madaraka, lakini ulishutumiwa kwa kuburuza miguu katika suala la kusitisha uanachama wa nchi hiyo baada ya ukandamizaji uliosababisha kumwaga damu dhidi ya waandamanaji uliofanywa na jeshi la Sudan.

Baraza la amani na usalama la Umoja wa Afrika limesema kuhamisha madaraka kwa mamlaka itakayoongozwa na raia, ni njia pekee itakayoruhusu Sudan, kuondoka kutoka katika mzozo wa sasa.Majeshi ya usalama yamewauwa waandamanaji kadhaa siku ya Jumatatu, katika matumizi makubwa ya nguvu nchini humo tangu kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir kulazimishwa kuondoka madarakani mwezi Aprili.

Siku ya Jumatano, idadi ya vifo iliyokadiriwa na upinzani kutokana na ukandamizaji huo ilipanda hadi watu 108. Umwagaji damu huo umeshutumiwa vikali na Umoja wa na mataifa ya magharibi


Like it? Share with your friends!

0