Sudan yafunga mipaka yake na Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati


0

Serikali ya mpito nchini Sudan imeamuru kufungwa mara moja mipaka ya nchi hiyo na mataifa ya Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati, kwa sababu ya vitisho vya ulinzi na uchumi ambavyo hata hivyo haikuvianisha.

Taarifa iliyotolewa na Baraza Tawala la Mpito nchini humo imesema vyombo vya moto vimekuwa vikivuka kiyume cha sheria mipaka na nchi hizo mbili zinazokabuliwa na machafuko.

Uamuzi huo unafuatia mkutano kati ya baraza la mpito na Serikali ya jimbo la Darfur Kusini, lililo sehemu ya eneo la magharibi ya Sudan la Darfur ambalo linakabiliwa na machafuko tangu mwaka 2003.

Mara kadhaa Sudan imelalamika juu ya uingizwaji wa silaha kwa njia za magedno kupitia mipaka yake na Libya na Jamhuri ya Afrika ya Kati ambazo hazina udhibiti wa mipaka yake kutokana na uwepo kwa mizozo.


Like it? Share with your friends!

0