SUARES: Sitashangilia nikibahatika kuwafunga Liverpool leo


0

Mchezo wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kati ya Liverpool na Barcelona, utachezwa tena leo katika dimba la Anfield, ikiwa ni marudio baada ya mchezo wa kwanza kumalizika pale Camp Nou Mei 01 mwaka huu.

Liverpool anakuwa mwenyeji wa Barca akiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa jumla ya magoli 3-0, ambapo Luis Suarez, raia wa Uruguay alihusika kwa kupachika nyavuni balo la kwanza na alionekana kufurahia zaidi goli lile licha ya kuwa Liverpool ilikuwa mwajiri wake kabla ya Barcelona.

Kitendo cha Suarez kushangilia goli lake pale Camp Nou, kiliwashangaza wengi kwani siyo kawaida wachezaji walio wengi kushangilia goli pale wanapoifunga klabu ambayo wametoka.

Hata hivyo kuelekea mchezo wa marudiano leo ambapo Liverpool atakuwa nyumbani akimkaribisha Barcelona, Suarez amesema endapo atabahatika kupachika bao tena, basi hatoshangilia kama alivyoshangilia pale Camp Nou Mei 01 2019.

Suarez aliondoka Liverpool mwaka 2014 na kwenda kuitumikia klabu ya  Barcelona ambako amedumu mpaka leo.

 


Like it? Share with your friends!

0