Spika Ndugai ataja ugumu wa kazi yake


0

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amesema watu wanapaswa kujua ugumu wa kuwa na wadhifa wa uspika na kuwataka wajifunze kuchuja baadhi ya maneno yanayowekwa katika mitandao ya kijamii kwa sababu mengi si ya kweli.

Ndugai ametoa kauli hiyo alipokuwa  katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi iliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), usharika wa Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

Spika Ndugai alijikuta anatoa kauli hiyo baada ya Askofu Dk Fredrick Shoo, kuwataka viongozi kutumia mamlaka yao vizuri, huku akimnyooshea kidole Spika Ndugai

“Nafikiri baba Askofu (Dk Fredrick Shoo- mkuu wa KKKT) umeona ugumu wa kuwa spika, umejaribu tu kidogo umeona wewe mwenyewe shughuli iliyotokea.”

“Kwa hiyo mnaposema kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Ndugai mjue kazi ngumu niliyonayo,” amesema Ndugai.

Akizungumzia tabia ya baadhi ya watu kumuandika vibaya Dk.Mengi, amesema hata wao hukumbwa na mambo hayo akiwataka watu kutoamini kila kinachoandikwa katika mitandao hiyo.

“Ujumbe huu ni kwa Watanzania na kwa baba zetu wapaka mafuta wa bwana siyo vyote mnavyovisoma ni kweli, ni vizuri pale ambapo mna mashaka kidogo basi mkatuuliza.” amesema Spika Job Ndugai.


Like it? Share with your friends!

0