Sita wauawa na meya wa Mogadishu kujeruhiwa


0

Watu sita wameuawa na meya wa Mogadishu amejeruhiwa kufuatia shambulio la bomu katika ofisi ya meya huyo wa mji mkuu wa Somalia.

Kundi la la al-Shabab limedai kuhusika na shambulio hilo likisema lilikuwa likimlenga mjumbe wa Umoja wa Mataifa. Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa James Swan, alikutana na meya Abdirahman Omar Osman, lakini aliwahi kuondoka kabla ya kuripuliwa bomu hilo.

Maafisa wa usalama wanachunguza shambulio hilo. Mji wa Mgadishu mara kwa mara umekuwa ukishambuliwa na kundi la al-Shabab, ambalo kwa zaidi ya muongo mzima limekuwa likipambana kutaka kuipindua Serikali ya Somalia.

Jumatatu iliyopita, mji huo ulishambuliwa kwa bomu lingine lilotengwa ndani ya gari na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine kadhaa kujeruhiwa.


Like it? Share with your friends!

0