Serikali yaziunganisha TPB na TIB


-1
-1 points

TANZANIA

Serikali imeziunganisha rasmi Benki ya Posta Tanzania (TPB) na Benki ya Maendeleo (TIB) kuanzia leo, baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuridhia, lengo likiwa ni kuwa benki moja imara ya biashara.

Uamuzi huo umefanywa kwa mujibu wa Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya 2006, kifungu kidogo cha 30 ambapo sasa, TPB itachukua mali na madeni yote ya TIB kuanzia leo Juni Mosi mwaka huu.

 

Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka amesema uamuzi wa kuziunganisha benki hizo ni sehemu ya uboreshaji wa mashirika na taasisi za serikali kiutendaji, ili kuhakikisha yanakuwa na ufanisi na kupunguza gharama kadri inavyowezekana.

 

Anasema kuwa hatua ya kuziunganisha benki hizo inatarajiwa kuleta mageuzi makubwa katika sekta hiyo ikiwemo ya kiutendaji, kimfumo, kimuundo na taswira ya benki mpya ikiwa na lengo la kuhakikisha inaweza kushindana ipasavyo katika sekta ya fedha.


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points