Serikali yasitisha vibali vya uagizaji Sukari nje ya nchi


0

Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga ametangaza kusitisha vibali vya uagizaji Sukari nje ya nchi kwa wazalishaji wa ndani, badala yake Serikali itatumia kampuni nyingine kuagiza, huku akibainisha kuwa Sukari iliyopo ina uwezo wa kuhudumia walaji nchini mpaka mwezi Mei, 2019 lakini kuanzia Juni Serikali itaagiza tani 25,000 hadi 28,000 ili kusitokee uhaba.

Waziri Hasunga aliyasema hayo katika mkutano wa wadau wa sekta binafsi na wadau wa kilimo, ambapo amebainisha lengo la kufanya hivyo ni kuwataka wazalishaji kuongeza nguvu ya kuzalisha nchini, kwani tangu Serikali iliporuhusu uingizwaji wa Sukari kutoka nje, wazalishaji wa ndani wamebweteka na wanashindwa kuviendeleza viiwanda vilivyopo nchini.

Kufuatia hatua hiyo Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama wa Taasisi Binafsi(TPSF), Louis Accaro ameipongeza Serikali kwa kusitisha vibali hivyo, lakini ameiomba Serikali kuwaweka maafisa ugani chini ya Wizara ya Kilimo na sio wa TAMISEMI, kwani wanashindwa kufanya majukumu yao ipasavyo ikiwamo kuwasimamisha wakulima.


Like it? Share with your friends!

0