Serikali ya Zimbabwe yashindwa kutaja mahali Robert Mugabe atazikwa


0

Waziri wa habari wa Zimbabwe amesema mwili wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Robert Mugabe, utalazwa katika sehemu tatu tofauti katika mji mkuu wa Harare kwa ajili ya kupewa heshima ya kitaifa kabla ya kuzikwa Jumapili ijayo.

Mugabe alifariki Ijumaa iliyopita akiwa kwenye hospitali moja nchini Singapore. Alikuwa na umri wa miaka 95.

Waziri huyo, Monica Mutsvangwa amesema mwili wa Mugabe utawekwa katika uwanja wa michezo wa Rufaro siku ya Alhamisi na Ijumaa utakuwa kwenye uwanja wa michezo wa kitaifa.

Kwa mujibu wa Mutsvangwa, Jumamosi mwili wa kiongozi huyo utalazwa katika Ikulu.

Hata hivyo waziri huyo alisema Mugabe atazikwa Jumapili, lakini hakutaja mahala ambapo maziko yatafanyika, hali ambayo inaudhihirisha uvumi kwamba kuna hali ya kutokukubaliana kati ya familia yake na serikali juu ya suala hilo.


Like it? Share with your friends!

0