Serikali kuchunguza Wakuu wa Mikoa, Madiwani na Wabunge wa mikoa 12


0

Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini inaanza kufanya shughuli ya uhakiki wa mgongano wa maslahi ya viongozi katika mikoa 12.

Hayo yamebainishwa leo kupitia taarifa iliyotolewa na Kamishna wa Maadili, Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma, Jaji mstaafu, Harold Nsekela.

Katika taarifa hiyo, Jaji Nsekela ametaja mikoa itakayohusika kwa viongozi wake kufuatilia ambayo  ni; Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Geita, Kagera, Mara, Mwanza, Dodoma, Tabora, Singida, Dar es Salaam na Shinyanga.

Amesema suala  hilo ni la kawaida kwa sababu sekretarieti ilianzishwa ili kusimamia mienendo na tabia ya viongozi wa umma, pamoja na utekelezaji wa Sheria ya maadili ya viongozi wa umma Na. 13 ya mwaka 1995 pamoja na marekebisho yake.

“Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma inatoa wito kwa wote ambao watahusika katika shughuli hii kutoa ushirikiano ili kufanikisha zoezi hilo.” Inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Akifafanua zaidi, Mkuu wa Habari na Mawasiliano ya Umma wa Sekretarieti ya Maadili, Honoratus Ishengoma amesema miongoni mwa viongozi watakaokwenda kuhakikiwa ni madiwani, wabunge na wakuu wa mikoa


Like it? Share with your friends!

0