Rwanda kupima Wazee COVID-19


0

Waziri wa afya nchini Rwanda amezindua huduma ya kupima COVID 19 kwa wazee na watu walio na magonjwa hatarishi katika wilaya ya Rusizi iliyopo magharibi mwa Rwanda.

Eneo hilo ambalo lipo karibu na mpaka wa nchi ya Juamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa maeneo machache ambayo yametangaza visa vipya vya maambukizi ya corona.

Baadhi ya maeneo katika wilaya hiyo tayari yamewekewa amri ya kutotoka nje tangu June 4 mwaka huu ili kuzuia kuenea zaidi kwa virusi.


Wizara imejitolea siku tatu za kupima wazee katika wilaya hiyo ya Rusizi baada ya tafiti kuonesha kuwa watu wenye umri wa kuanzia miaka 60 na kuendelea wapo katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya COVID 19.

Lakini pia watafanya vipimo vya COVID 19 kwa watu ambao wanamagonjwa mengine kama vile kisukari na magonjwa sugu ya kupumua

Upimaji utaanza katika maeneo yaliyowekwa marufuku ya kutotoka nje na utaendelea katika maeneo mengine nchini ikiwa maambukizi yatazidi kuongezeka.

Wizara ya afya nchini humo imeweka maabara katika wilaya Rusizi ili kuhakikisha majibu yanatoka kwa haraka


Like it? Share with your friends!

0