Ripoti ya Umoja wa Mataifa yaitolea macho Tanzania


1
1 point

Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Haki za Binadamu, Michelle Bachelet ameelezea kuzorota kwa haki hizo hapa nchini. 

Katika taarifa yake iliyowasilishwa mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja huo, Bachelet amesema kupitishwa kwa sheria ya usimamizi wa tasisi zisizo za kiserikali (NGO) Juni, mwaka huu, ni miongoni mwa sababu zinazochochea kuzorota huko, kwani sheria hiyo huenda ikaminya uhuru wa asasi hizo.

Hata hivyo, ripoti hiyo imepongeza juhudi za Serikali katika kupambana na rushwa na kutekeleza miradi ya afya na elimu.

Ndani ya ripoti hiyo, serikali imekumbushwa kuwa uhuru wa kujieleza, kupata habari na kukusanyika ni nyenzo muhimu katika utekelezaji wa misingi ya utawala bora

Aidha, ripoti hiyo imegusia kukamatwa kwa wanahabari na kushikiliwa kwa muda mrefu na jeshi la polisi.


Like it? Share with your friends!

1
1 point