Ripoti ya Mabadiliko ya tabia nchi yatoa tahadhari


0

Kundi la viongozi wa kibiashara, kisiasa na kisayansi limesema uwekezaji mkubwa katika kuzingatia mabadiliko ya tabianchi katika muongo ujao utaleta manufaa makubwa huku mataifa yakijiepusha na hasara kubwa na kuimarisha chumi zao.

Tume ya kimataifa ya marekebisho inayojumuisha watu maarufu ikiwa ni pamoja na bilionea Bill Gates na aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban-Ki-moon, imetoa ripoti ya kuzihimiza serikali na makampuni duniani kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi mbali na kujaribu kukabiliana nazo. Ripoti hiyo inapendekeza kuwekeza dola trilioni 1.9 kati ya mwaka 2020 na 2030 katika sekta kama mifumo ya mapema ya tahadhari, miundombinu ambayo inaweza kustahimili viwango vya bahari vinavyoongezeka na hali mbaya ya hewa na pia kuimarisha sekta ya kilimo kuweza kustahimili ukame


Like it? Share with your friends!

0