Rais wa zamani wa Ufaransa afariki


0

Rais wa zamani wa Ufaransa, Jacques Chirac amefariki dunia leo akiwa na umri wa miaka 86.

Mwanasiasa huyo amefariki akiwa amezungukwa na watu wa familia yake, mapema hii leo, na inaelezwa kuwa hali yake ya Afya ilidhoofika tangu alipopata mardhi ya Kiharusi mwaka 2005 akiwa madarakani

Chirac alifuata siasa za mlengo wa wastani,huku akiiongoza Ufaransa kuanzia mwaka 1995 hadi 2007.

Alihudumu kama meya wa jiji la Paris na aliwahi kuwa Waziri Mkuu wa ufaransa mara mbili kabla ya kuwa rais wa nchi hiyo


Like it? Share with your friends!

0