Rais Magufuli awaonya Kamanda wa Polisi na Mkuu wa TAKUKURU Arusha


0

Dar es Salaam, Tanzania

Rais John Pombe Magufuli leo amemuapisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha mteule, Idd Kimanta anayechukua nafasi ya aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo baada ya uteuzi wake kutenguliwa.
Lakini pia ameshuhudia uapisho wa wakuu wa wilaya, ACP Jotham Balele wa Monduli, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongosi na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Bakari Msulwa uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
June 19,2020 Rais Magufuli, alitangaza kutengua nafasi za viongozi wa Jiji la Arusha akiwemo Mkuu wa Mkoa Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya Gabriel Daqarro na Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Arusha na Kuteua Viongozi wapya ambao leo wamepishwa
Katika halfa ya Uapisho huo, Rais Magufuli anaweka wazi sababu ya Kutengua Uteuzi wa vingozi wa Arusha kuwa ni kutokuwa na maelewano baina yao.

“Mtakumbuka hivi karibuni Arusha imebidi nitengua uteuzi wa wote niliokuwa nimewateua kuanzia RC, Mkurugenzi wa mji pamoja DC ni kwa sababu katika kipindi karibu cha miaka miwili walikuwa wanagombana tu, kila mmoja ni bosi kila mmoja anatengenza mizengwe ya mwenzake sikufurahishwa” alisema Rais Magufuli
Rais Magufuli anabainisha kuwa Ugomvi wao ulikuwa ukiwacheleweshea wananchi wa Arusha kupata maendeleo ikiwemo stendi nzuri.
Ameenda Mbali zaidi na kueleza kuwa tatizo la migogoro Arusha lililetwa na aliyekuwa mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo.

“Tatizo hili lililetwa na Mkuu wa Mkoa Arusha (Gambo) anazungumza hivi huku, anazungumza hivi kule lengo ni kuonekana yeye ni mzuri sana, tusitoe ahadi ambazo haziwezekani” alisema Rais Magufuli.
Hata hivyo ametoa onyo kwa mkuu wa TAKUKURU Arusha na Kamanda wa Polisi mkoani Arusha Jonathan Shana kutokana na kufanya kazi ambazo hazihusiani na nafasi zao za kazi.

 

 


Like it? Share with your friends!

0