Rais afanya mabadiliko JKT, ateua bosi mpya


-1
-1 points

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mabadiliko madogo ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa

Akitangaza mabadiliko hayo, Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo ametangaza mabadiliko hayo madogo ambapo Brigedia Jenerali Charles Mbughe amepandishwa cheo na kua Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa

Kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo akipokea mikoba ya Meja Jenerali Martin Busungu ambaye sasa anakua Mkuu wa Tawi la Jeshi la Akiba, Mbughe alipandishwa cheo kutoka kua Kanali na kuwa Brigedia Jenerali kwa kile kilichobainishwa kwamba ni kazi nzuri aliyoifanya katika usimamizi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa majengo ya serikali mkoani Dodoma.


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points