Rais aahidi kutowatupa Walimu


0

DODOMA

Rais John Magufuli amesema moja ya vipaumbele vya serikali ni kukuza na kuimarisha sekta ya elimu nchini, hasa katika kuboresha na kupanua wigo wa upatikanaji wake kuanzia ngazi ya awali hadi elimu ya juu.

Ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama Cha Walimu Tanzania-CWT leo hii, uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako.

Rais Magufuli amesema baada ya uhakiki uliofanywa na serikali, watumishi 306,917 wamepandishwa vyeo, 160,367 miongoni mwao wakiwa ni walimu.

Amesema, katika kipindi cha mwaka huu wa fedha, serikali inatarajia kuwapandisha vyeo watumishi wengine 290,625 wakiwemo walimu 166,548

Kwenye hotuba yake, Rais Magufuli amesema hatowatupa walimu, kwani anafahamu shida zao na ndio maana aliendelea kuwalipa mshahara hata shule zilipofungwa kutokana na janga la corona

 


Like it? Share with your friends!

0