Putin kung’oka madarakani akiwa kikongwe


0

URUSI

Rais wa urusi Vladimir Putin (67) ameshinda kura ya maoni itakayomuwezesha kubaki madarakani hadi mwaka 2036 akiwa na miaka 83.
Hatua hiyo imefikiwa kutokana na asilimia 78 ya kura zilizopigwa, ikiwa ni asilimia 90 ya kura zilizohesabiwa, kwa mujibu wa tume ya uchaguzi ya Urusi.
Putin amekuwa madarakani katika wadhifa wa urais na pia Waziri Mkuu kwa miaka 20 na kwa hivi sasa ni Rais aliyehudumu nchini Urusi kwa kipindi kirefu zaidi.
Kura ya maoni ilitaka kuidhinishwa kwa mabadiliko ya Katiba yatakayomuwezesha Putin kugombea tena katika uchaguzi mara mbili zaidi.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Urusi, Ella Pamfilova amesema muhula wake wa hivi sasa unamalizika miaka minne ijayo.
Putin amejijengea umaarufu kuwa ni mlinzi na kiongozi anayeleta uthabiti nchini humo, kinyume na hali ya kuyumba kwa uchumi na kisiasa katika kipindi cha baada ya iliyokuwa Jamhuri ya Kisovieti katika miaka ya 1990, ikiwa ni kabla ya kuingia kwake madarakani.
Putin, mrithi aliyeteuliwa na Rais wa kwanza wa Urusi, Boris Yeltisin, ameshinda chaguzi zote nne za urais, katika mwaka 2000, 2004, 2012 na 2018, kwa wingi mkubwa.
Yamekuwa mabadiliko makubwa ya Katiba ya Urusi tangu kuanza kutumika mwaka 1993 kufuatia kuvunjika kwa Umoja wa Kisoviet.

 


Like it? Share with your friends!

0