Prof Kabudi na Katibu Mkuu wa UN, wajadili suala la amani


-1
-1 points

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi, jana amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres kuhusiana na suala la amani na usalama katika nchi za ukanda wa Maziwa Makuu.

Profesa Kabudi yuko New York nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu la 74 la Umoja wa Mataifa.

Viongozi hao walijadili kwa upana kuhusu Tanzania na nchi zingine za ukanda wa Maziwa Makuu.

Taarifa kutoka Umoja wa Mataifa zinaeleza kuwa Profesa Kabudi na Guterres walijadili kuhusiana na hali ya usalama katika nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).

Guterres katika mazungumzo hayo aliishukuru Tanzania kwa jitihada zake za kuzuia machafuko kwa kulinda amani ndani na nje ya nchi.

Kabla ya mkutano huo Profesa Kabudi pia alikutana na Rais Dinald Trump wa Marekani. Hata hivyo, taarifa kuhusu mazungumzo yao hazijatolewa hadharani.

 


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points