Polisi wawapigia magoti waandamanaji Marekani


-1
-1 points

Baadhi ya waandamanaji nchini Marekani wameonesha kufurahishwa na kitendo cha maafisa wa polisi kupiga magoti pamoja nao, ikiwa ni ishara ya amani katika vuguvugu la maandamano linaloendelea nchini humo.

Maandamano hayo yamefanyika kwa siku kadhaa sasa ikiwa ni ishara ya kupinga mauaji Mmarekani mweusi, George Floyd.

Wakati maeneo mengine nchini humo yakishuhudiwa polisi wakitumia nguvu na mabomu ya machozi kutawanya waandamanaji, jijini New York mambo ni tofauti baada ya polisi kuungana na waandamanaji.

Video mbalimali katika mitandao ya kijamii zinaonesha namna polisi katika jiji hilo wakipiga magoti, huku sauti za waandamanaji zikisika kufurahia kitendo hicho.

Kwa mujibu wa mtandao wa CNN, miongoni mwa waandamanaji wamesikika wakisema hawakutegemea kuona kitendo hicho cha polisi na kwamba ni jambo tofauti na walivyozoea.

 

Wanasema kuwa hiyo ni dalili nzuri, lakini bado wanaendelea kuangalia namna mamlaka zitakavyochukua hatua

Jumamosi iliyopita, maafisa wengine wa polisi walipiga magoti na kusali pamoja na waandamanaji, mbele ya jengo la kihistoria la Coral Gables.

Na katika jimbo la Michigan, Afisa mmoja wa polisi, Chris Swanson aliungana na kutembea pamoja na waandamanaji waliokuwa wakiimba ‘tembea na sisi’ huku na yeye akisema ‘twende twende’ kisha akawauliza, ‘wapi mnataka tuelekee, tutatembea usiku wote,’ kitendo hicho kilizua shangwe kwa waandamanaji

Maandamano katika jiji la New York yamekuwa yakifanyika kwa amani tofauti na miji mingine nchini humo.

 


Like it? Share with your friends!

-1
-1 points