Polisi waelimisha jamii kuhusu COVID-19


0

Baadhi ya wananchi jijini Dar es Salaam wanasema elimu wanayoipata kuhusu COVID – 19 kutoka kikosi cha usalama barabarani cha jeshi la polisi katika vituo vya usafiri wa umma, inaongeza kiwango cha ushiriki wao kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona.

katika kituo cha mabasi yaendayo kasi kilichopo Kivukoni jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha elimu, mafunzo na uenezi cha usalama barabarani, Abel Swai, akitoa elimu kwa abiria wanaosubiri usafiri kituoni hapo.

Miongoni mwa msisitizo wake ni kuhusu uvaaji sahihi wa barakoa, matumizi ya vitakasa mikono na watu kupeana nafasi wanapoketi ama kusimama,  ili wasisongamane hasa kwenye foleni wakati wakisubiri usafiri

“Kuanzia mwezi wa tatu wizara ya afya ilitupa darasa elekezi na baada ya hapo tukawa walimu wa kujikinga na ugonjwa wa corona katika vyombo vya usafiri” alisema Abel Swai

Wanatumia njia gari la polisi ambayo inaspika, matangazo yanayoelezea Corona pamoja na vipaza sauti kuongea na wananchi ana kwa ana.

Kwanza TV inaongea na baadhi ya wananchi kituoni hapo ambapo wanasema elimu hiyo inawakumbusha kufuata kanuni zilizowekwa na wizara ya afya katika kujikinga na virusi vya corona.

Swai anasema changamoto iliyopo ni kuwa abiria wanaokutana nao muda uliopo si sawa na wale watakaokutnana nao baada ya saa mbili kupita lakini wanajitahidi kwa kushirikiana na UDART na Wizara ya Afya kuhakikisha elimu inawafikia wote

Na kila anapomaliza kutoa elimu hupenda kujihakikishia kutoka kwa wananchi kama kweli wameelewa somo alilotoa.

Swai anatoa wito kwa makamanda wa polisi nchi nzima kuendelea kutoa elimu katika maeneo mbalimbali ya utendaji wa kazi ili kuimbukusha jamii juu ya kujikinga na virusi vya corona.


Like it? Share with your friends!

0