Papa Fransics abusu miguu ya viongozi mahasimu nchini Sudan


0

Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis, amefanya tendo la unyenyekevu na ambalo halikutarajiwa baada ya kupiga magoti na kubusu miguu ya viongozi wanaohasimiana nchini Sudan Kusini, kuwahamasisha kuuendeleza mchakato wa amani.

Mwishoni mwa ziara ya kiroho ya siku mbili ya viongozi hao wa Afrika mjini Vatican, Papa Francis alimuomba Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir pamoja na hasimu wake Rieck Machar, kuendeleza mazungumzo ya amani  licha ya ugumu unaoendelea kujitokeza.

Papa Fransic hufanya tendo hilo la kitamaduni na la kiimani la kuwaosha miguu wafungwa siku ya Alhamisi kuu, lakini hajawahi kufanya tendo kwa viongozi wa kisiasa.

Alisema mwishoni mwa ziara hiyo kwamba anataraji kusitishwa kwa uadui, mapigano, mgawanyiko wa kikabila na kurejeshwa kwa hali ya amani nchini humo.

 

 


Like it? Share with your friends!

0