Uncategorized

Ofisi tume ya kupambana na Rushwa Zimbabwe zafungwa kufuatia COVID 19


1
1 point

Tume ya kupambana na rushwa nchini Zimbabwe (ZACC) imefunga ofisi zake za makao makuu baada ya mume na mtoto wa mmoja wa wafanyakazi wake kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Hapo awali ripoti zilionesha kuwa mfanyakazi huyo ameathirika na Virusi hivyo lakini msemaji wa tume John Makamure alisema hakuna tatizo kwani sio yeye bali ni mume wake na mtoto.

Msemaji huyo anasema kuwa walimpima mfanyakazi huyo na hakuwa ameambukizea virusi hivyo.

Anasema ofisi hiyo imezingatia kanuni za kujikinga na COVID 19 na wafanyakazi kutoka wizara ya afya na watoto wamepuliza dawa katika ofisi hiyo hivyo imefungwa kwa muda na itakuwa tayari kwa matumizi baada ya saa 48

Hata hivyo amesema kufuatia ongezeko la visa vipya vya COVID 19 Wizara ya afya imeongeza kampeni za uhamasishaji katika jamii juu ya ugonjwa huo kwa kutumia miongozo ya WHO.

Mpaka sasa Zimbabwe ina jumla ya kesi 525 zilizothibitishwa pamoja na vifo sita huku waliopona wakiwa ni 64.


Like it? Share with your friends!

1
1 point