Odinga amshauri Rais Magufuli kushirikiana na viongozi dhidi ya COVID-19


0

Waziri Mkuu wa zamani ambaye pia ni kinara wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, amesema janga la virusi vya corona linatakiwa kujadiliwa kwa kina na viongozi wa ukanda wa Afrika Mashariki, kwani lisipodhitiwa katika nchi moja litaathiri nchi zingine zilizokatika ukanda huo.

Hayo ameyasema wakati wa mahojiano maalumu na kituo cha utangazaji cha BBC, akidai nchi moja haiwezi kupata tatizo bila kuathiri nyingine katika ukanda huo.

Odinga ambaye pia ni Kiongozi wa chama cha upinzani cha Orange Democratic Movement (ODM)  anasema anatilia shaka mwitikio wa Rais John Magufuli dhidi ya janga la corona na kudai kuwa anahitaji kushauriana na viongozi wenzake katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Ameongeza kuwa ameona Rais Magufuli akitilia shaka vifaa vya upimaji nchini Tanzania, kwamba havitoi majibu sahihi lakini angependa kumwambia kuwa kama watu wanaathirika na kupoteza uhai basi ajue kuna tatizo.

Odinga, anasema amejaribu kumpigia simu Rais Magufuli lakini hakufanikiwa kumpata na amemuachia ujumbe, lakini angependa  kumshauri kuwa akae na viongozi wenzake na atapewa ushauri mzuri ambao anajua ataufuata.


Like it? Share with your friends!

0