Nigeria yaondoa vizuizi kwenye nyumba za ibada


0

Kano, Nigeria

Kikosi kazi kilichoteuliwa na Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria kwa ajili ya kupambana na janga la virusi vya corona, kimetangaza hatua kadhaa za kulegeza vizuizi vilivyotokana na janga hilo kuanzia leo.
Imeelezwa kuwa sehemu zitakazolegezewa vizuizi hivyo ni pamoja na maeneo ya ibada.
Boss Mustapha, ambaye ni mfanyakazi mwandamizi wa serikali nchini Nigeria, amesema kuwa mji wa Kano Kaskazini mwa nchi hiyo utaanza kulegeza hatua yake ya kuwazuwia watu kutoka nje kuanzia leo Jumanne.

Boss Mustapha, ambaye ni mfanyakazi mwandamizi wa serikali nchini Nigeria, amesema kuwa mji wa Kano Kaskazini mwa nchi hiyo utaanza kulegeza hatua yake ya kuwazuwia watu kutoka nje kuanzia leo Jumanne.

Safari za ndege nazo huenda zikaanza kuanzia Juni 21, mwaka huu huku makali yakiongezwa katika amri ya kutotembea usiku iliyowekwa nchi nzima kuanzia saa 4 usiku hadi saa kumi alfajiri kutoka muda uliopo sasa wa saa mbili usiku hadi saa 12 asubuhi.
Mratibu wa taifa wa kikosi kazi cha kupambana na COVID-19, Sani Aliyu , amesema sekta ya fedha nchini humo itaanza kurejea katika muda wake wa kawaida wa kazi.

Nigeria nchi yenye wakazi wengi barani Afrika na ambako ukristo na uislamu una waumini wengi, imeorodhesha visa 10,162 vya maambukizi ya virusi vya corona na vifo 287.

 


Like it? Share with your friends!

0