Nchi masikini kukumbwa na baa la njaa


0

Umoja wa Mataifa (UN) umeomba dola bilioni 4.7 za nyongeza kwa ajili ya kuwalinda mamilioni ya watu waliopo kwenye mataifa yenye hali mbaya zaidi, wakati huu wa mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Naibu Katibu Mkuu wa umoja huo anayeshughulikia masuala ya kibinaadamu, Mark Lowcock, amesema machungu makubwa zaidi ya janga la COVID-19 yatakuwa kwa nchi masikini zaidi, na kwamba bila ya kuchukuwa hatua madhubuti hivi sasa, dunia ijitayarishe kwa ongezeko la migogoro, njaa na umasikini.

Fedha hizo ni tofauti na dola bilioni 2 ilizoziomba wakati wa kuzindua mpango wa huduma za kibinaadamu Machi 25, mwaka huu ambapo hadi sasa, UN imekusanya nusu ya kiwango hicho.

Idadi kamili ya dola hizo bilioni 6.7 zinatazamiwa kugharamia mpango wa huduma za kibinaadamu kufikia Disemba mwaka huu.


Like it? Share with your friends!

0