Nasari apigania ubunge wake mahakamani


0

Aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nasari, ameanza safari ya kupigania ubunge wake ambao alivuliwa na Spika wa Bunge Job Ndugai, kwa makosa ya kutohudhuria mikutano mitatu mfululizo ya Bunge.

Kwa mujibu wa taarifa aliyoituma Joshua Nassari amesema Marchi 18, 2019 ndiyo alifungua shauri katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, kupinga hatua hiyo ya Spika ya kumvua ubunge.

Aidha taarifa yake imesema kuwa kesi hiyo imesogezwa mbele hadi Machi 26, kwa ajili ya upande wa Mwanasheria Mkuu kupeleka majibu ya madai ya msingi ya washtaki, na Machi 27 kesi hiyo itaanza kusikilizwa.

Aidha Mbunge huyo ameeleza wameomba kuwekwa kwa zuio la Mahakama, kwamba kusifanyike uchaguzi mdogo kwenye jimbo hilo hadi pale kesi ya msingi itakapokamilika.


Like it? Share with your friends!

0